TEZI DUME NA TIBA YAKE

 ⚕️FAHAMU DALILI,MADHARA NA TIBA YA KUVIMBA KWA TEZI DUME.



+255679039663

Dr Hamza majombo

www.majombo.com

 

◼️Tezi Dume (Prostate gland) ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).


➡️▪Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. 

 ➡️▪BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.


DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI DUME(BPH)


Dalili  hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote;-

▪️Hukojoa mkojo unaokatika katika

▪️Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu

▪️Husita kabla ya kuanza kukojoa

▪️Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara

▪️Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe

▪️Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu

hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku

▪️Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)

Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH.


MADHARA YA KUVIMBA KWA TEZI DUME(BPH) NI PAMOJA NA;-


◼️Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)

◼️Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo

◼️Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo

◼️Maambukizi katika njia ya mkojo (UTI)

◼️Madhara katika figo au kibofu

◼️Shinikizo la damu

◼️Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)

◼️Maambukizi mbalimbali

◼️Nimonia (Pneumonia)

◼️Damu kuganda

◼️Uhanithi


          🦴VIPIMO NA UCHUNGUZI🦴


    ▪️Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na;-

◼️Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE)

◼️Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. 

◼️Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.

Kipimo cha kuchunguza ◼️kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.


Kwa elimu zaidi wasiliana na 

🍄Dr.Hamza majombo

🍄+255679039663

🍄www.majombo.com

Comments