JINSI YA KUANDAA MKATE WA KOROSHO


 1️⃣ *NAMNA YA KUANDAA MKATE WA KOROSHO KWA WAGONJWA WA ACID REFLUX, VIDONDA VYA TUMBO & GASTRITIS*

⤵️⤵️⤵️⤵️⤵️⤵️⤵️


*VIUNGO/INGREDIENTS*


1.🖇️  2/3 kikombe cha unga wa korosho

2.🖇️ 1/4 kikombe cha unga wa nazi

3.🖇️ 1/4 kikombe cha mbegu za chia

4.🖇️ 1/4 kikombe cha maji

5.🖇️ Mayai 2

6.🖇️ 1/2 kijiko cha chai (tsp) chumvi

7.🖇️ 1/2 kijiko cha chai(tsp) baking soda



*MAANDALIZI:*⤵️

1.🖇️ Preheat oven hadi JOTO LA 180 Celsius.


2.🖇️ Changanya unga wa korosho, unga wa nazi, mbegu za chia, baking soda, na chumvi pamoja.


3.🖇️ Ongeza maji na mayai, na changanya vizuri hadi uwe na mchanganyiko mzuri(Homogeneous mixer).


5.🖇️ Weka mchanganyiko wa mkate kwenye tray yenye karatasi ya kupikia, na weka tray hiyo kwenye oven/JIKO


6.🖇️ Pika mkate kwa dakika 20-25 hadi uwe na rangi ya dhahabu(golden colour)


7.🖇️ Ondoa mkate kutoka kwenye oven/jiko na uache upoe kabisa kabla ya kukata vipande.


*Pia unaweza kuongeza viungo kama vile bizari, tangawizi, au vitunguu saumu ili kuongeza ladha yake.*


⚫ Mkate huu wa korosho unaweza kutumiwa kama mbadala wa mkate wa kawaida katika.


⚫ Unaweza kula vipande vyake kama chakula cha ASUBUHI, MCHANA AU JIONI.


⚫ *MKATE HUU UNASHIBISHA SANA NA UNAKATA HAMU YA KULA KULA MARA KWA MARA KWASABABU UNA KIASI KINGI CHA MAFUTA NA KIASI KIDOGO SANA CHA WANGA.*

Comments