IJUE U.T.I NA MADHARA YAKE MAKUBWA
_________________________________
🛟Je! U.T.I ni nini?🛟
U.T.I ni kifupisho cha neno URINARY TRACT INFECTION.
maana yake,Maambukizi katika mfumo wa mkojo.
Hapa tunapata jibu moja kwa moja kwamba. U.T.I sio ugonjwa flani bali ni mkusanyiko wa maambukizi yanayojitokeza katika mfumo wa mkojo.
__________________________________
__________________________________
🪗AINA ZA U.T.I🪗
__________________________________
Aina kuu za ugonjwa huu zipo mbili. Upper na Lower.maana yake mashambulizi upande wa juu na wa chini katika mfumo wa mkojo.
CYSTITIS – Maambukizi katika kibofu.
Aina hii inajumuisha mkusanyiko wa maambukizi yanayojitokeza upande wa chini wa mfumo wa mkojo.
URETHRITIS– Maambukizi katika mrija unaopisha mkojo. .
PYELONEPHRITIS– Maambukizi katika figo.mara nyingi hapa vichujio vya damu kwenye figo hushambuliwa na kupeleka maradhi mbalimbali ya figo.
VAGINITIS– Maambukizi katika baadhi ya sehemu za uke.
📌Maradhi haya huwaathiri na kuwashambulia zaidi wanawake kuliko wanaume.Na hii ni kutokana na mfumo wa maumbile yao.
Moja kati ya vitu vinavyosahaulika zaidi ni ukaribu wa matundu matatu ya sehemu za siri za wanawake. Yaani tundu la mkojo,tundu la ukke(eneo la kujamiana) pamoja na tundu la haja kubwa. Ukaribu huu mkunwa unasababish a wadudu kuhama au uchafu kuhama kiwepesi na kuingia eneo ambalo sio lake.
WADUDU MAARUFU KWA KUSABABISHA U.T.I
Wadudu wanaoambukiza au kusababisha U.T.I mara kwa mara ni BAKTERIA ingawa FUNGI(fangasi ) nao wana uwezo wa kusababisha huu ugonjwa.baadhi ya wadudu hawa ni......
1. Escherichia coli.
2. Klebsiella pneumoniae.
3. Proteus mirabilis.
4. Enterococcus faecalis.
5. Staphylococcus saprophyticus.
Ingawa *Escherichia coli* (E.COLI) ndio maarufu zaidi kwa kusababisha maambukizi haya zaidi ya wadudu wengine hao.
_________________________________
🫧DALILI KUU ZA U.T.I🫧
@ Maumivu wakati wa kukojoa.
@ Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu.
@ Damu kuonekana katika mkojo.
@ Kukojoa mkojo wenye rangi ya chai.
@ Kukojoa mkojo wenye harufu kali.
@ Maumivu ya kiuno kwa wanawake zaidi.
@ Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume na wanawake mara chache.
@ Maumivu ya maeneo ya juu ya mgongo.
@ Homa zisizo na mpangilio.
@ Kusikia baridi mara kwa mara.
@ Kusikia kichefuchefu baadhi ya mida.
@ Mwili kuishiwa nguvu.
@ Maumivu upande wa kulia na kushoto chini ya mbavu.
@ Maumivu ndani ya uke na uume.
@ Maumivu kwenye kitovu.
.....................................................
❄️MADHARA YA U.T.I❄️
🚨 Husababisha kuvimba kwa Tezi dume kwa wanaume.
🚨 Husababisha magonjwa ya kudumu ya figo na hatimae figo kufeli.
🚨 Husababisha mwanamke kuharibikiwa kizazi na hatimae kutoshika mimba.
🚨 Huharibu misuli na mishipa inayozuia mkojo na kupelekea mkojo kutoka wenyewe.
🚨 Maumivu ya mgongo na nyonga.
🚨 Kupoteza hamu ya tendo.
🚨 Kupoteza nguvu za kiume.
🚨 Mvurugiko wa vichocheo.
Yapo mengi sana ya kuelezea juu ya ugonjwa huu ila kwa leo niishie hapa.
Najulikana kama..
+255 679039663
+255 742633692
Dr.Hamza majombo.
Majombo herbal clinic
Mbagala-Dar es salaam
Comments
Post a Comment