ZIJUE FAIDA ZA KITUNGUU SAUMU NA TANGAWIZI KWA AFYA YAKO.
+255679039663
Dr.Hamza majombo
Katika maisha ya sasa, ni
vizuri sana kujua kila
unachokula kina faida au
madhara gani mwilini
mwako, kwani unachokula
leo, ndicho
kitakachokufanya uugue au
uwe mzima kesho, tiba au
madhara ya chakula
hujijenga mwilini
kidogokidogo na matokeo
yake huonekana baada ya
muda mrefu.
Kitunguu saumu kimekuwa
kikitumika kama dawa ya
mitishamba, takribani
miaka 5,000 iliyopita.
Historia inaonesha kuwa
wafungwa wa nchini China
walikuwa wanatakiwa kula
kitunguu saumu kibichi kila
siku asubuhi ili kuimarisha
afya zao.
Aidha inaelezwa zaidi kuwa
nchini Misri, watumwa
walikuwa wakilishwa
vitunguu saumu na
vitunguu maji ili wapate
nguvu za kujenga ‘ma
piramid’.
Vile vile vitunguu vilikuwa vinatumika kama
dawa ya kufukuza majini na
mapepo wabaya.
Ukiacha ushahidi huo wa
kiasili kuhusu uwezo na
umuhimu wa kitunguu
saumu kiafya, utafiti wa
kisayansi umegundua pia
kuwa kishina kimoja cha
kitunguu saumu kina dawa
sawa na uniti 100,000 za
vidonge vya Pennicillin
ambayo ni karibu ya robo
dozi ya vidonge hivyo na
havina madhara yoyote
katika mwili wa binadamu.
Kitunguu saumu
kinaaminika kuwa na
uwezo wa kuzuia aina
mbalimbali za saratani,
kama vile saratani ya
tumbo, ngozi, matiti, koo
na utumbo mkubwa.
Aidha kitunguu saumu kina
uwezo wa kudhibiti seli
zisizaliane vibaya na kuleta
madhara mengine mwilini.
Aidha, kitunguu saumu kina
uwezo wa kushusha
shinikizo la juu la damu, ili
kupata matokeo yake katika
kuponya maradhi hayo,
unahitaji kuwa unakula
angalau kitunguu saumu
kimoja mpaka vitatu kila
siku kwa muda wa miezi
mitatu. Lakini hata
utakapokula kiasi chochote
utakachoweza kwa wale
msio na maradhi yoyote,
bila shaka mtakuwa
mnajijengea kinga katika
miili yenu.
Aidha ulaji wa vitunguu
saumu vibichi, husaidia
kurekeshi kiwango cha
sukari kwa wagonjwa wa
kisukari na manufaa
yanapatikana zaidi kwenye
vitunguu vibichi kuliko vya
kupika au kukaanga.
Vilevile unaweza
kuchanganya asali na
vitunguu saumu na kula
pamoja kama dawa ya
kuondoa mafua.
TANGAWIZI
Hii nayo ni dawa ya
mitishamba yenye nguvu
na maarufu sana nchini
China, India na Japan.
Imekuwa ikitumika katika
nchi hizo kwa karne kadhaa
na kuenea hadi Mashariki
ya Kati, Spain na West
Indies. Kwa mujibu wa
historia yake, kwa mara ya
kwanza Tangawizi
ilitengenezwa nchini
Jamaika ili kusaidia tatizo
la ukosefu wa choo,
kichefuchefu, ugonjwa
unaotokana na kutembea
kwa muda mrefu na uchovu
wa asubuhi.
Tangawizi inaaminika kuwa
na uwezo wa kuzuia
kuchafuka kwa tumbo,
kubana kwa kifua na
kuumwa kwa kichwa. Kwa
mujibu wa kitabu cha You
Are What You Eat, katika
bara la Asia, Tangawizi
hutumika kuogea ili
kuponya tatizo la kuziba
kwa pua kutokana na mtu
kuwa na ‘aleji’.
Tangawizi
husagwa na unga wake
kutumika kuandaa kinywaji
au inaweza kutumika ikiwa
bado mbichi kwa kuwekwa
kwenye maji ya moto na
kunywa.kinga ni Bora kuliko Tiba.
Comments
Post a Comment